Header Ads

LightBlog

Karibu katika blogu ya Ndimara Tegambwage

Karibu uwanja mpya wa mawazo.

12 comments

Ansbert Ngurumo said...

Karibu katika uwanja wa blogu. Utakutana na wengi hapa wenye shauku ya uhuru; wapambanaji kama wewe. Tunakujua. Karibu, uwe chachu ya harakati.

Jeff Msangi said...

Karibu uwanjani tulicheze goma kwa pamoja.Uhuru

Ndesanjo Macha said...

Ndimara,
Fikra zangu bila wewe hazingekuwa zimekamilika. Wewe nakuita mwalimu wangu. Pale Wakati Ni Huu, nakumbuka. Ulikuwa mkali. Ulikuwa na jicho kali. Ulitaka tuandike kama waandishi na sio wapita njia. Nakumbuka. Na tena nashukuru.

Ila furaha zaidi ni kuona umeingia humu. Umejiunga nasi. Vita dijitali. Tutapigania haki ya kujieleza hadi huku kwenye Intaneti. Sijui watakimbilia wapi walaghai hawa na suti zao na magari yanayolindwa na polisi, ving'ora, yanayopita mitaani mbio kama vile mwizi anakimbia toka eneo la wizi!

Karibu!

Said Michael said...

Kwa mikono miwili tunakupokea katika uwanja huru wa kutoa mawazo kwa uhuru zaidi. Karibu

Unknown said...

Kaka Ndimara Tegambwage sio? Hakuna mpenda watu kama huyu, na hapendi kijinga anapenda kwa vile anajua maana yake. Bila watu hakuna uhai.ANAANDIKA KWA MAPENZI HAYO. Nilifanya kazi na Ndimara gazeti la Uhuru enzi hizo ndiyo naanza, mwaka 1976. Akatukaribisha mi na vijana wengine, uwanjani. Kaiva huyu bwana. Anafahamu mengi na kuingia kwake blogini ni fahari na furaha. Anastahili kupigiwa madebe. Waandishi kama hawa ni wachache sana na wanahitajika sana si tu Tanzania, duniani.

Bob Sankofa said...

Tumekata mzizi wa fitina, wazee hawana pa kujificha. Ule msemo wao wa "Hii teknolojia ni kwa vijana" hauna nafasi tena.

Asante kwa kuukata mzizi wa fitina baba yangu Ndimara. Karibu sana.

Rama Msangi said...

Nimeishiwa na maneno kwakweli, maana hisia zangu juu ya ujio wako mzee Ndimara, ni zaidi ya kile ninachoweza kukisema. Labda niseme tu karibu sana. Tuko pamoja na naamini hata JUMUWATA sasa imempata kamanda wa aina yake.

Rama Msangi said...

Nimeishiwa na maneno kwakweli, maana hisia zangu juu ya ujio wako mzee Ndimara, ni zaidi ya kile ninachoweza kukisema. Labda niseme tu karibu sana. Tuko pamoja na naamini hata JUMUWATA sasa imempata kamanda wa aina yake.

Simon Kitururu said...

Karibu sana !

Vempin Media Tanzania said...

Karibu mzee natambua sana kwamba wewe ni mtu makini tulikusoma tangia enzi zile tuko sekondari riwaya yako ya duka la kaya kwa hakika umekuwa chachu humu blogini kwetu. Karibu usiishie mlangoni ingia ndani kabisa ya kijiji chetu hiki, tupo wengi huku kuna wengi wa ajabu ajabu hivi!

Ansbert Ngurumo said...

Mheshimiwa,
Inasemekana bado upo mlangoni, hujaingia ndani yay blogu. Ni kweli? Unatafutwa. Na mahali penyewe na kukutana na watu ni ndani ya blogu.

ndimara tegambwage said...

Kuna waliokataa kunifungulia. Nikaamua kupiga teke mlango. Lakini haukuvunjika. Sasa nimo ndani na mlango nimeuacha wazi kwa kila anayetaka kuingia.

Napenda kuwashukuru nyote kwa kunikaribisha. Tuwe pamoja. Nielekeze mtakapoona kuna haja ya kufanya hivyo. Uwezo wa kuelewa haraka ninao. Nia ipo pia. Twende kazini.

Powered by Blogger.