Barabara ya Dar es Salaam iliyoleta ugomvi
Jana tarehe 8/8/217 niliokoa vijana wawili wasitoane macho na
kung’oana meno. Nilikuta wamekabana koo. Nikaamuru dereva wangu asimame.
Wakati ninatoka katika gari, wakawa ndio wanaangushana chini na
kuanza kuviringishana kwenye vumbi huku wakipigana ngumi kichwani.
Ilichukua kama dakika tano hivi kuwaachanisha. Nikauliza
kilichowasibu.
Mmoja akasema: “…huyu ni mpumbavu. Anasema kuwa barabara hii ilikuwa
ya lami lakini sasa ni udongo mtupu. Mimi nikamwambia haiwezekani lami itoke
kiasi cha kubaki vumbi namna hii; lakini yeye anabisha. Ndipo tukashikana…”
Mwingine akasema: “…hili jinga tu. Mimi nimekuwa nikipita barabara
hii kwa miaka mitano sasa nikienda shule. Ilikuwa ya udongo; baadaye wakaweka
lami. Sasa lami imekwisha yote katika kipindi cha miaka mitatu hivi na imerudia
hali ileile ya vumbi.
“Huyu (aliyekuwa akipigana naye) hakuwepo hapa lakini anabisha na
kuanza kunitukana na kusema kuwa lami haiwezi kuisha katika kipindi hicho. Ndio
umekuta tumekamatana lakini ni kutokana na huyu kunitukana.”
“Barabara ya Ugomvi” ni ile inayochomoka kwenye Barabara ya
Shekilango, Sinza Afrika Sana kupitia Kituo cha Polisi cha Kijitonyama jijini
Dar es Salaam.
Ni kweli, barabara hii ilikuwa vumbi wakati wa jua na matope wakati
wa mvua. Wakaweka kifusi (sijui nani!). Baadaye wakaweka lami (sijui nani) ikateleza
na karibu dunia yote ikahamia huko. Leo ni vumbi tupu.
Je, unaweza kusaidia kuoroshesha visababishi vya ugomvi huu wa
kung’oana meno na macho? Barabara yenyewe ni hii katika picha.
No comments
Post a Comment