Hawakuandikishwa: wameachwa au wamekataa?
Kila mwananchi ana haki ya kujiadikisha ili aweze
kushiriki uchaguzi katika eneo lake - Oktoba 2015.
WOTE AMBAO HAWAKUANDIKISHWA
KATIKA DAFTARI LA WAPIGAKURA
WAWEZA KUJITOKEZA KUPITIA HAPA
WOTE AMBAO HAWAKUANDIKISHWA
KATIKA DAFTARI LA WAPIGAKURA
WAWEZA KUJITOKEZA KUPITIA HAPA
Kwenye mawasiliano ya imeili mjadala unaendelea. Waandishi wa habari na wasio waandishi wanakusanya majina ya watu ambao hawakuandikishwa katika daftari la kupiga kura - kwa sababu zozote zile - katika maeneo ambako tayari Tume ya Uchaguzi imetangaza kuwa imekamilisha uandikishaji. TUWAFAHAMU WAO NA IDADI YAO. NAO WAFAHAMIANE.
Je, wewe unajua nani hakuandikishwa au anadai kutoandikishwa katika eneo lako? Tupe taarifa kwa mtindo huu hapa:
Unachoombwa kufanya:
1. Sikiliza.
2. Pata anayedai kuwa hakuandikishwa.
3. Pata majina yake matatu.
4. Pata anakoishi na anwani yake/simu yake.
5. Pata kitambulisho chake chochote – kama kipo.
6. Pata maelezo: Kwanini hakuandikishwa/mazingira.
7. Rekodi/nukuu kauli anazodai kuambiwa na waandikishaji.
8. Kama simu yako ina kamera, pata picha yake.
9. Peleka taarifa zako kwa:
ndimara2014@gmail.com
10. Kwa maulizo zaidi ita: 0713 61 48 72.
Maelekezo yaliyopelekwa kwa waandishi wa habari na wadau wa habari sehemu mbalimbali nchini ni kama ifuatavyo:
Kuwa Jicho, Sikio na Mdomo
wa Jamii
OKTOBA mwaka huu (2015) kutakuwa na Uchaguzi Mkuu – kuchagua
madiwani, wabunge na rais. Hivi sasa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) inafanya kazi
ya kuandikisha wapigakura.
Tayari Tume imetangaza kumaliza kazi ya kuandikisha
wapigakura katika baadhi ya wilaya; LAKINI tangazo hilo linafuatiwa mgongoni na
sauti nyingi za wananchi wanaodai kuwa hawakuandikishwa.
Nani hakuandikishwa? Yuko
wapi? Ana maelezo yapi kuhusu kutoandikishwa?
Katika eneo unamoishi au uliko sasa kikazi au kwa matembezi,
kuna wananchi wanaodai kuwa Tume haikuwaandikisha. Wangependa kuandikishwa ili
washiriki kuchagua viongozi wanaoona watawatumikia; au watakaowawajibisha pale
watakaposhindwa kuwahudumia.
Moja ya kazi kuu za mwandishi wa habari ni kupaza sauti za wananchi; ili
wanachofikiri, wanachotaka, wanachosema na wanachotenda au kutendewa, kiweze kusikika
kwa wengine, wakiwemo wenye mamlaka na dola kwa jumla.
Ukiwa jicho la nyongeza la jamii; sikio la nyongeza la jamii;
na mdomo wa nyongeza wa jamii; sasa tafuta na kurekodi, kwa manufaa ya umma na
watawala; watu wote katika eneo ulipo au unakokwenda, ambao kilio chao ni
kutoadikishwa.
Siyo rahisi kuorodhesha kila mmoja ambaye anadai kutoandikishwa;
lakini una uwezo wa kufikia hadi watu 50 au zaidi ili kuweka ushahidi unaoweza
kusaidia kuleta utatuzi na hata mabadiliko makubwa katika jamii. Ni heshima
iliyoje kuwa mmoja wa vibarua wa umma na kutambuliwa hivyo!
Tuko waandishi saba. Tunakushirikisha wewe na mwishoni mwa
kazi hii ya kujituma kukutana na wenyekilio na kukusanya taarifa hizi, utakuwa
tayari sehemu ya kundi hili.
Haya ni mazingira yaliyosheheni FURSA za kuinua na kuibua vipaji
vya waandishi wa habari. Ni fursa za kutumikia umma kwa njia ya kurekodi
ukweli, tena kuurekodi kwa usahihi; ili wahusika waweze kuchukua hatua. Ni
fursa zinazozaa, kulea na kukomaza umahiri katika taaluma ya habari.
Unachoombwa kufanya:
1. Sikiliza.
2. Pata anayedai kuwa hakuandikishwa.
3. Pata majina yake matatu.
4. Pata anakoishi na anwani yake/simu
yake.
5. Pata kitambulisho chake chochote –
kama kipo.
6. Pata maelezo: Kwanini
hakuandikishwa/mazingira.
7. Rekodi kauli anazodai kuambiwa na
waandikishaji.
8. Kama simu yako ina kamera, pata picha
yake.
Peleka taarifa zako kwa ndimara2014@gmail.com
10.
Kwa
maulizo ita: 0713 61 48 72.
Asanteni,
Ndimara Tegambwage
No comments
Post a Comment