Header Ads

LightBlog
SENGONDO WETU

Angalia pale...
Machozi yawatiririka
Makamasi yawachuruzika
Miili yawaka, yapoa:
Mara jasho lawakamuka
Mara mitima yaganda
Na vinywa kuwakauka.
Hayo nami yanikumba.

Hawakai, hawalali, hawatulii
Hawaoni, hawasikii, hawakubali
Dunia bila Sengondo:
Katika familia
Katika madarasa
Katika mahakama
Katika urafiki na maongezi?
Walomjua Sengondo
Kwa mapishi darasani,
Mijadalani na nyumbani -
Sikiliza
Soma
Pekua
Sengondo alijiandaa kutokufa.
Panga limezika mwili tu;
Na tutalia kumkosa
Bali alotenda yatadumu.

ndimara.

No comments

Powered by Blogger.