Header Ads

LightBlog

WASIRA KATUMWA AU KAPAYUKA?

Kazi ya Usalama wa Taifa ni nini (TISS)?

Waziri wa mahusiano Ikulu, Steven Wassira amefanya kazi nzuri bila kujua. Ni wakati alipouliza, mjini Dodoma, “Kibanda ni nani” hadi afanyiwe unyama kama aliofanyiwa.
1.  Kauli ya Wassira imeonyesha kuwa KWELI Idara ya Usalama wa Taifa "hushughulikia" watu fulani; jambo ambalo wamekuwa na kigugumizi kusema. Sasa amelitoa. Ambalo hakusema ni kushughulikia namna gani; lakini inaonyesha ni kama alivyofanyiwa Absalom Kiband, mhariri mkuu wa New Habari Corporation na mwenyekiti wa Jukwaa la Wahari – kupigwa, kung’olewa meno, kucha, kutobolewa jicho…
2. Wassira amesema Idara ya Usalama wa Taifa inaweza kushughulikia watu kama Dk. Slaa na Freeman Mbowe – viongozi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema). Hakueleza kwanini; lakini tunajua ni kwa kuwa wanataka kushika madaraka – kuyatoa mikononi mwa CCM. Hili linazaa jambo lingine; kwamba
3. Sasa yeyote kati ya hao wawili atakayejikwaa, sharti tumtafute Wassira. Yawezekana hili lilimtoka kwa bahati mbaya au alikuwa na ghadhabu; lakini tayari tunalo. Kwamba hawa ndio lengo la idara ya usalama wa taifa na si mwingine, angalau kwa sasa.
4. Lakini uwindaji haumo katika Chadema peke yao. Upo pia ndani ya CCM. Tuweke masikio tayari kusikia ni akina nani ndani ya CCM ambao wataelekezewa usalama wa taifa kwa kuwa hawako pamoja na mrengo mkuu. Chanzo chetu, bila shaka, kitakuwa Wassira.
5. Sasa Kibanda ni nani? Anauliza. Tusimpe jibu. Tuseme tu kwa sasa, kwamba, kama usalama wa taifa wana uwezo wa kushughulikia wakubwa, sembuse wadogo kama Kibanda. Tumwachie Wassira kazi ya kumweka Kibanda pale anapoweza kumweka au aulize usalama wa taifa ambao wanaweza kumwambia mara moja.
6. Tusilokuwa na uhakika nalo ni kama Wassira alitumwa kuweka hadharani kwamba Slaa na Mbowe wanaandaliwa "kitu" na usalama wa taifa. Yawezekana amepayuka, jambo ambalo linaweza kumweka pabaya; au kaagizwa na hivyo atapewa nishani kwa “ujasiri” wa kutoboa siri.
7. Tusubiri. Tutaona.
ndimara

2 comments

salutary said...

HAKIKA MH.MBOWE NA DR. SLAA YAWAPASA KUJIAPANGA NA WAWEZE KUMCHUKULI HATUA ZA KISHERIA NDG. STEVEN WASSIRA ALIYESEMA HADHARANI NA OFFICIALLY HASA BUNGENI KWAMBA SERIKALI,CCM NA UASALAMA WA TAIFA WANAWATAFUTA (TARGETED) DR.SLAA NA FREEMAN MBOWE.
AIDHA KWA LOLOTE LITAKALOWATOKEA HAWA VIONGOZI WAKUU WAWILI WA CHADEMA TUJUE WATAKUWA WAMESHUGHULIKIWA NA USALAMA WA TAIFA KWA SABABU TU WANATAKA KUITOA CCM MADARAKANI... NA PIA KWA MAELEZO YA WASSIRA TAYARI TUMEKWISHAJULISHWA RASMI NA KUHAKIKISHWA YA KWAMBA USALAMA WA TAIFA WANAFANYA KAZI KWA MAELELKEZO YA CCM.

Powered by Blogger.