Header Ads

LightBlog

Mjadala juu ya Rais Yahya Jammeh wa Gambia kunyonga watu 40

KIFO SIYO ADHABU ni UHALIFU MWINGINE

Posted to forum: mabadilikotanzania@googlegroups.com,    Tuesday, 21 August 2012

Naona kuna mkondo wa kuua. Sasa tuachane na wanaharakati na watetezi wa haki za binadamu. Tujaribu kufikiri bila vivuli vyao. Twende kwenye hoja ya kuua:

ANAYEUA ANASTAHILI KUUAWA. Hicho ndicho kilio cha wachangiaji wengi. Kapoku kamuua Sadoko. Sasa wanataka Kapoku auawe. Wanataka mahakama iamue kuwa Kapoku auawe mpaka afe. Mahakama inaamua hivyo. Serikali inayosimamia utekelezaji inatoa panga, msumeno, kamba au umeme na kuua Kapoku. Nani sasa ameua Kapoku? Kwa ufupi mchinjaji ni serikali/utawala.

Twende mbele. Hoja ya wachangiaji wengi ni kwamba ANAYEUA AUAWE. Hivyo serikali iuawe. Kuua ni kuua - awe ameua masikini au tajiri, mtu binafsi au serikali. Ni uharamia tu.

Tutafute adhabu kwa aliyeua. KIFO SIYO ADHABU. Kifo ni kuondosha maisha ya yule ambaye angefanya adhabu. Tena angefanya adhabu angejutia alichofanya, angejifunza na jamii ingejifunza. Aliyekufa hajifunzi. Hajutii kosa lake. Kama Kapoku ameondoa maisha ya Sadoko na serikali imeondoa maisha ya Kapoku; hakika wote ni WAUAJI. Si vema kuishi katika dunia ya wauaji.

ndi.

No comments

Powered by Blogger.