MEMBE, LOWASSA & SITTA
Mjadala juu ya kauli za Lowassa, Membe na Sitta kuhusu vita na Malawi:
1. Tukubaliane na kujiridhisha kuwa
Kikwete-Sitta-Lowassa-Membe walikuwa wamekubalinana. Matamshi yanalenga
kutangaza vita kati ya Tanzania na Malawi. Wasingeweza kuyatoa hivyo
kilevilevi. Kilichokuwa kinasubiriwa ni amri ya Amiri Jeshi kuamuru majeshi kusogea/kwenda
uwanjani:
(a) Wasingekuwa
wamekubaliana, hivi sasa wasingekuwa na kazi kwa kujaribu kuingiza nchi vitani
bila idhini ya Bunge na, au mkuu wa majeshi.
(b) Membe ni mtu
wa karibu sana na rais - "tarishi wa kidiplomasia" asiyetakiwa kwenda
kinyume sana na mwajiri.
(c) Lowassa ni
Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Ulinzi - anashirikisha mhimili mwingine
(Bunge) na hapaswi kuropoka kama hakuna mjadala nyuma ya pazia.
(d) Sitta ni
waziri wa mahusiano ya kimataifa ya Afrika Mashariki ambaye ana nafasi ileile
ya Membe, uzito wa waziri wa muda mrefu na mwandani anayekaimu nafasi ya waziri
mkuu bungeni.
2. hata hivyo, katika mazingira ya sasa ya utawala wa
Kikwete, kuna ukimya hata pale ambapo maisha ya wananchi yako hatarini. Yawezekana
pia walikuwa wanajaribu kina cha maji huku wakisema, kama hali itaonekana
kutibuka, rais ambaye ni "mwenye kauli ya juu" (siyo ya mwisho),
ndiye atatoa msimamo. Tayari ameutoa.
3. Yawezekana pia kauli ya Kikwete ikawa sahihi ingawa siyo
kweli: Kwamba "ni kelele za wapinzani." Hakika Sitta, Lowassa na
Membe wanatajwa kwenye orodha ya washindani wa tiketi ya urais kupitia CCM.
Siyo wapinzani wa CCM, bali wanapingana wao kwa wao na wangependa kuonyesha
nani mwenye msuli katika "kulinda nchi" pindi ikiingia mgogoro.
4. Ni ubabe wa kipuuzi unaopuuza kekima na historia na
unaodharau ushauri na juhudi za amani. Hapa Mtoi ana pointi.
ndi.
No comments
Post a Comment