Header Ads

LightBlog

JINSI YA KUPATA HARAKA MADAKTARI BINGWA WENGI


Wanahitajika haraka madaktari bingwa nchi nzima
Waliopo hawatoshi. Simama hapo:

Waliopo ni wangapi
Lini walianza kuwa wachache
Lini walianza kuonekana kuwa wachache
Lini walikuwa wachache

Wito ni kuhamisha waliopo katika hospitali kubwa kwa mgao maalum
Ili angalau pembe zote za nchi ziweze kuonja huduma za mabingwa. Simama hapo:

Wanahitajika madaktari wangapi kwa nchi nzima
Hao waliopo wamekuwa wakifanyaje kazi zao
Nani wamekuwa wanahudumia sehemu nyingine nchini
Wahitaji wote wamekuwa wakipelekwa hospitali kubwa zilizopo
Wahitaji wamekuwa wakifuatwa huko waliko
Wahitaji wamekuwa wakifa kwa kukosa huduma ya kitabibu ya madaktari bingwa

Wito kupunguza usafirishaji mbali wahitaji hadi hospitali zenye madaktari bingwa
Kupunguza idadi ya vifo kwa kutopata huduma ya kitaalam ya mabingwa. Simama hapo:

Waliokuwa wakisafirishwa kwenda hospitali zenye mabingwa ni wangapi
Hospitali zipi/ngapi zimekuwa zikilundikiwa wahitaji
Idadi ya wahitaji kwa kila hospitali yenye mabingwa - kwa miaka mitatu mfululizo hadi 2017
Mafanikio ya hospitali katika kukabili mlundikano wa wahitaji
Matatizo ya hospitali katika kukabili wingi wa wahitaji
Changamoto zinazokabili hospitali na wahitaji
Changamoto za madaktari bingwa binafsi/kitaaluma
Waliokufa kutokana na:
              umbali hadi hospitali yenye daktari bingwa
              uchache wa madaktari bingwa
              matatizo/changamoto zinazokabili hospitali zenye madaktari bingwa

Wito wa kuongeza madaktari bingwa kwa njia ya mafunzo. Simama hapo:
Himiza wanafinzi kusoma sayansi
Chagiza wanafunzi kusomea udaktari
Uhimizaji/uchagizaji umekuwepo kwa muda gani
Muda wa kosomea udaktari
Muda hadi kuwa bingwa - wa kuaminiwa
Mbinu za kuchagiza watarajiwa
Jinsi ya kuajiri
Jinsi ya kutunza madaktari bingwa wa zamani - waliopo
Jinsi ya kulea, kukuza na kutunza madaktari wapya
Jinsi ya madaktari bingwa wa sasa na wajao/wapya kujitunza na kubaki kazini (mazingira)

Yuko wapi msaidizi wa daktari bingwa kwa miaka 5, 10 au 15
Hajawa daktari bingwa
Hana elimu ya kutosha
Hana ujuzi
Hana uzoefu
Amekuwa anakwenda tu - mbumbumbu bado
Hana stadi
Hana mbinu
Hajajiendeleza
Bado yupo palepale akisubiri kukuliwa na wanaotoka shule/vyuo

Nani anafikiria mbinu mbadala za kupata madaktari bingwa
Zile za kuangalia waliomo
Kuibua waliomo
Kukuza waliomo
Kuongeza uwezo wa waliomo kuliko kusubiri wa vidato
Kuliko kuazima kutoka nje
Kuliko kutanua idadi isiyotanuka

Yuko wapi mwandishi wa habari
Yule mwandishi mtekenyaji!
Aliyemwona muhusika na kumuuliza haya
Na kumtaka ajibu/afafanue kwa jamii kuona na kusikia. Simama hapo:

                Ili kukumbusha umuhimu wa kufikiri
                Ili kuchagiza jinsi ya kufikiri tofauti
                Ili kuibua fikra mbadala
                Ili kuondokana na mawazo yaleyale juu ya tatizo lilelile
                Kuondokana na njia zilezile za utatuzi wa tatizo/changamoto ileile isiyotatulika
Ili kupata majibu na suluhisho la kweli na sahihi.

(Andishi hili lilitumiwa darasani jijini Dar es Salaam wiki hii kufikirisha waandishi wanapokwenda kufanya mahojiano)

               

              
             

No comments

Powered by Blogger.