tag:blogger.com,1999:blog-8943712461165130839.post743653637318984916..comments2023-09-19T01:07:34.015-07:00Comments on Uhuru Hauna Kikomo: DC AKISHINDWA SERIKALI IMESHINDWAndimara tegambwagehttp://www.blogger.com/profile/05750977914976705256noreply@blogger.comBlogger1125tag:blogger.com,1999:blog-8943712461165130839.post-30077410098607827822009-10-08T01:42:52.756-07:002009-10-08T01:42:52.756-07:00Ndg Mwandishi wa makala haya, kwanza nikupongeze k...Ndg Mwandishi wa makala haya, kwanza nikupongeze kwa mtiririko mzuri wa uchambuzi huu.

Pili niseme wazi kuwa siyo tu Uhahula peke yake ndio haelewi au kutotambua wafugaji na ufugaji wao, bali serikali hii kwa ujumla; wanasema "hakuna wafugaji Tanzania bali kuna Wachungaji"! Ni jambo la kusikitisha kuona kuwa serikali haiwajali Wafugaji kiasi cha kutishia kufuta ufugaji! Embu ajaribu kutishia kufuta kilimo aone cha mtema kuni!

Nachozungumzia hapa nikwamba WAFUGAJI wa nchi hii wamekuwa wakinyanyaswa sana na serikali mpaka kufikia hatua serikali ikatamka wazi kuwa wafugaji warudi kwao walikotoka kana kwamba wametokea kuzimuni wakaibukia ghafla Tanzania!

Mzee wetu Ndimara, kaelezea vizuri sana kuhusu wafugaji na ufugaji wao kuwa ndio maisha yao, uhai wao na kila kitu bila ufugaji kwao maisha ni bure.

Wafugaji ni wazalendo wa nchi hii wana haki sawa na stahiki kama mkulima, wafanyabiashara wa Kariakoo na tena zaidi ya wawekezaji wabovu na matapeli wanaokumbatiwa na serikali kwa sababu wanazozijua wao.

Aidha kuna dhana potofu iliyozuka na tunafahamu ilikoanzia kuwa WAFUGAJI ni waharibifu wa mazingira, lakini swali la kujiuliza tena rahisi la darasa la pili B; Wafugaji hawakuanza leo kufuga Tanzania, walikuwepo hata kabla ya ukoloni mpaka leo, walikuwa wakihama na makundi makubwa ya mifugo, SWALI: Kama ni waharibifu wa mazingira na vyanzo vya maji, nchi hii si ingekuwa JANGWA? Wanyama wanaotegemea nyasi na maji ambao pia wanaishi na hao wafugaji nao pia si wangetoweka? Je tungekua na urithi wa kujivunia kuwa nasi tuna wanyamapori? Kwa wale waliotembelea mbuga za Ngorongoro watanielewa nachozungumza! Huko Wafugaji na mifugo yao wanaishi pamoja na wanyama na hakuna uharibifu wa mazingira ulotokea. Tujifunze kutoka huko, tusiongee na kuandika tu bila kufanya tafiti( No Research No Right to Speak)!

Nakupongeza tena mwandishi wa makala haya kwa kutambua ukandamizaji, udhalilishwaji na uonevu unaofanywa dhidi ya wafugaji wazalendo na wenye haki zote za kuishi na kuendeleza maisha na ufugaji wao katika nchi yao.

Gideon Sanago.Jameshttps://www.blogger.com/profile/10308443796562228209noreply@blogger.com