SITAKI
Wasioona tatizo la Mkuchika, sheria
Na Ndimara Tegambwage
SITAKI kuwa mchoyo. Someni wanavyosema baadhi tu ya wasomaji wa uchambuzi wangu juu ya hatua ya serikali ya kufungia gazeti la KuliKoni iliyochapishwa kwenye ukurasa huu Jumapili iliyopita.
Hadi jana saa tatu asubuhi, jumla ya wasomaji 127 walikuwa wameandika ujumbe mfupi wa simu na 39 wamepiga simu. Asilimia 99.7 wanapinga serikali kwa hatua iliyochukua. Someni kwa furaha:
Naungana na mada yako leo. Mimi nilidhani wanaposikia habari mbaya zinazoliletea taifa aibu, basi ni wakati mzuri wa kufundisha jamii juu ya kuishi kwa maadili mazuri, siyo kumfungia mtoa taarifa. Hii ni aibu kwa kiongozi aliyepewa dhamana – 0712-752595.
Pole na hongera kwa kuchagua kuelimisha jamii juu ya kufungiwa kwa KuliKoni – 0717-664685.
Ni kweli. Jeshi walikanusha asubuhi ileile habari ilipotoka hata bila kufanya uchunguzi wala kuomba undani wa habari ili wafanyie kazi (usianike namba yangu).
Hongera kwa article yako. Hivi waziri (George Mkuchika, wa Habari, Utamaduni na Michezo) anajua mavazi ya watoto wa kike vyuo vikuu? Majumbani nako amefika? – 0713-243231.
Mashaka yangu ni pengine waziri hajui istlahi uchi ina maana gani; uchi kwa mujibu wa nani, tatizo picha za uchi au uchi wenyewe? Kama watembea uchi wamo katika ibada je, picha za uchi magazetini ndio kero kuu ya wananchi Tanzania? – 0713-326376.
Tatizo kuu kabisa la wanaoitwa viongozi wetu, ni UNAFIKI. Kujikataa ndiyo uswahili wenyewe na utamaduni wa taifa. Inasikitisha. Inafedhehesha. Inadharaulisha. Reason na logical thinking havipewi nafasi kuchanua. Nakuomba endelea kuandika akina Mkuchika wapungue – 0754-532797.
Dawa ya kufungia gazeti ni kumpa kibano aliyelifungia kama ilivyokuwa kwa MwanaHALISI. Mbona safari hii kama hamumwoni? Mwasubiri nini? Kazi njema – 0787- 155882.
Nimesoma uchambuzi wako. Umenifurahisha kwa kuwa umeongea ukweli – 0716-455073.
Mungu akupe nguvu na hekima zaidi. Waandishi kama wewe mnapigwa vita lakini Mungu yupo upande wetu; amekushika kwa mkono wake wa kuume; hautatetereka. Songa mbele. A luta continua – 0715-808283.
Nimekusoma. Viongozi wetu hawakai hata siku moja wakasoma magazeti na kuchambua. Magazeti yanajaribu kuwakumbusha wakuu wetu kuwa taifa maadili hakuna…lakini leo gazeti la kurekebisha uozo waziri analifungia. Kisa? Limesema mitihani imeibwa.
Tunakwenda wapi? Wanataka magazeti yaandike kibaka kaiba kuku; lakini wakiandika wakubwa wamechota mabilioni ya shilingi, huo ni uchochezi…Tunaenda kubaya sana – 0765-938181.
Nimesoma makala yao. Umenikuna. Endelea hivyo. Tutafika. Gerald wa Kyela – 0767-481431.
Ndugu mwandishi, nakuombea kwa Mwenyezi Mungu uendelee na karama yako uliopewa na Mungu. By Masunga kutoka kijiji cha Mwasayi wilayani Maswa – 0787-229774.
Una kila sababu ya kuungwa mkono. Endelea. Wewe ni mpiganaji, una kila sababu ya kuungwa mkono – 0652-411969.
Vyombo vya habari vipo kwa ajili ya kuwajulisha wananchi habari za ukweli halisi ambazo wao ni vigumu kuzipata. Je, kuna ubaya gani wananchi kujua nchi yao inaelekea wapi?
Kufungiwa kwa KuliKoni na kufutwa kwa gazeti la Leo Tena ni kuvitisha vyombo…wakubwa wameamua kuhamishia hasira zao kwa wanyonge…Mkuchika amekurupuka. Mimi kama mwananchi sikubali – 0712-703631.
Umesema magazeti kama Leo Tena huwa yanajifuta yenyewe. Tukisubiri yajifute yenyewe yatakuwa yameshaharibu sana. Nina wasiwasi kama uliliona gazeti hilo – 0755-923565.
Sijui kama hujui kama yeye (Mkuchika) ni waziri mwenye dhamana…na majukumu yake ni “kuoversee” sekta ya habari. Naamini kwa uzoefu ulionao unajua kuwa ana kila mamlaka kufanya alichokifanya kwa mujibu wa sheria. Kwamba hukubaliani na sheria hiyo hakuna ubaya ni haki yako – 0655-280400.
Sasa inabidi ianzishwe wizara ya ufisadi na utamaduni wa mikataba; pia wizara ya kufuta magazeti na vyombo vyote vya habari -0713-442524.
Nimesoma makala yako. Mbona sioni mshikamano wenu wa hadhara wa kupinga kufungiwa magazeti? Wananchi twataka mtuongoze – 0713-280002.
Nimekupata (Mkuchika na sheria yake). Zamani Bushiri alimwambia Chakubanga alipoona anaficha bagi baada ya kuona polisi: Uliyokwishavuta vitendo vyake utavificha wapi? – 0713-234722.
Naungana na wewe 100% juu ya sheria na Mkuchika hasa aya ya 28: Huwezi kutumikia umma ambao umeufunga mdomo… – 0777-722382.
Wanahabari unganeni, msiandike habari zake hadi upite uchaguzi mkuu, Oktoba 2010 – 0714-768588.
Bravo. Hapo umempasha Mkuchika. Laiti na wanahabari wengine wangekuwa na ujasiri huo (usianike namba yangu).
Wamelifungia gazeti la KuliKoni lakini lengo lao ni MwanaHALISI, RAIA Mwema na Tanzania Daima. Je, kuna uhuru wa habari – 0718-122081.
Maoni ni mengi. Kila mmoja ana lake la kusema kadri anavyoguswa. Tujiulize: Je, waziri mmoja akijiuzulu, siyo kwa kashfa za ukwapuaji mabilioni ya shilingi benki kuu, bali kwa kukataa kutumikia sheria katili, itakuwaje?
Itakuwa hivi: Serikali itakumbushwa kuwa fimbo yake, iliyoweka ili kupigia nyoka pindi akitokea, sasa inatumika kupigia mume, mke na watoto. Itupwe. Hapana. Ivunjwevunjwe na kuwa kuni. Inanyang’anya haki. Inafedhehesha.
Sheria ya Magazeti ya mwaka 1976 ni kitanzi shingoni mwa hata mawaziri wenyewe pindi watokapo kwenye “utukufu” wa wizara hiyo au wa serikali. Ina tabia ya kuwasubiri wastaafu au wastaafishwe ndipo waone kuwa ni katili kupindukia.
Kinachosikitisha ni vipi watawala wameona utamu – tangu mwaka 1976 – wa kuendelea kuwafunga midomo na akili – wazazi wao, watoto wao, ndugu zao na jamii nzima ya Tanzania.
Kuna haja kwa Watanzania kufanya maamuzi: Kama hakuchi tufungue milango – alfajiri itukute nje katikati ya maandalizi mapya ya kutafuta haki. Na wewe umo.
O713-614872
ndimara@yahoo.com
www.ndimara.blogspot.com
Friday, May 21, 2010
POROJO ZA SERIKALI NA MISHAHARA YA WAFANYAKAZI
SITAKI
Porojo za serikali kuhusu mishahara
Na Ndimara Tegambwage
SITAKI waziri anayejifariji kwa kauli ndogo na rejareja hasa katika masuala yanayohitaji busara na hekima.
Anachokifanya Profesa Juma Kapuya, waziri wa kazi, ama kwa utashi binafsi au kwa kuagizwa na serikali, kinamuumbua na hata kuumbua serikali.
Wafanyakazi wamesema watafanya mgomo kuanzia 5 Mei mwaka huu kushinikiza serikali kushughulikia maslahi yao. Wamesema pia kwamba hawamwaliki rais kwenye sherehe zao za Mei Mosi mwaka huu.
Profesa Kapuya, kwa mizaha yake, akijua kuwa madai ya wafanyakazi ni nyongeza ya mishahara, amekurupuka na kusema mishahara katika sekta binafsi imeongezwa kwa asilimia 100.
Aliwaambia waandishi wa habari Jumanne iliyopita kwamba Mwanasheria Mkuu wa serikali atatangaza hivi karibuni, katika gazeti la serikali, ongezeko la asilimia 100 kwa mishahara katika sekta binafsi.
Serikali au Kapuya wanapata wapi ujasiri wa kuongeza mishahara ya sekta binafsi lakini wanashindwa kuongeza mishahara kwa watumishi wake? Wana uhakika gani kwa viwango hivyo vitalipwa na vinakubalika?
Kama Kapuya anasema nyongeza ya mishahara kwa watumishi wa serikali inahitaji majadiliano zaidi, kwa nini majadiliano hayo ya kina yasihitajike katika sekta binafsi inayolipa kodi serikalini?
Waziri wa kazi anasema mwanasheria “atatangaza hivi karibuni” nyongeza ya mishahara. Hivi karibuni ni lini hasa? Baada ya Mei Mosi? Kabla ya mgomo wa 5 Mei? Baada ya mgomo?
Kama serikali ina uwezo wa kuahidi kitu “hivi karibuni,” ilishindwa vipi kuchukua hatua muda wote tangu wafanyakazi wadai mafao na kufikia hatua ya kutaka kufanya mgomo?
Hili ndilo linafanya wengi wajenge mashaka juu ya nia na shabaha ya serikali. Au, kwa vile serikali inasema haishughulikii mishahara ya watumishi wake, basi itumie sekta binafsi kuepusha songombindo hili?
Hivi nani amemwambia Kapuya na serikali yake kwamba wafanyakazi wanataka “tangazo la mwanasheria mkuu” wa serikali? Tangazo ni la nini hasa? Mbona katika madai ya wafanyakazi hakuna tangazo?
Je, tangazo la mwasheria wa serikali linaloahidiwa “hivi karibuni,” likija kweli hivi karibuni na kusema mishahara itaongezwa lakini itakuwa mwaka kesho, litakuwa limekidhi haja ipi?
Kapuya na, au serikali, wameongea lini na wafanyabiashara, wenye viwanda na wakuu wa maeneo mbalimbali ya sekta binafsi?
Lini na wapi serikali ilikubaliana na watawala wa sekta binafsi kuwa kuanzia sasa walipe asilimia 100 ya mishahara ya wafanyakazi wake?
Lini serikali ilikutana na wafanyakazi au viongozi wake; kujadili kwa kina na kukubaliana kuwa hicho ndicho kiasi wanachotaka – siyo zaidi wala pungufu – na hivyo kuanzisha mijadala na waajiri?
Nani ameidanganya serikali kuwa inaweza kutoka usingizini wakati wowote; au inaweza kuchomoka katika fukuto la woga wa migomo ya wafanyakazi na kuamuru waajiri kutoa viwango vya mishahara kama inavyotaka?
Sasa baadhi ya waajiri katika sekta binafsi wameanza kusema kuwa hawataongeza mishahara. Wengine wanasema wanaweza kuongeza mishahara lakini itabidi wapunguze wafanyakazi.
Chama cha Waajiri Tanzania (ATE), kikiongea kupitia msemaji wao Aggrey Mlimuka kilieleza kidiplomasia juzi Ijumaa kuwa kinaangalia mwenendo huu na kuchunguza la kufanya.
Kwa vyovyote vile, sasa serikali imechokoza nyuki. Kwanza imeleta ubaguzi kwa kusema itatangaza mishahara kwa wafanyakazi wa sekta binafsi na kuwataka watumishi wake “kusubiri.”
Hivi hao watumishi wa serikali watasubiri hadi lini ili wapate angalao tangazo la kupandishiwa mishahara kinadharia kupitia mwanasheria mkuu wa serikali; achilia mbali kulipwa?
Pili, serikali imeingiza waajiri katika mgogoro wake. Nao wameanza kuitilia mashaka na kupinga hatua yake; siyo kwa kauli rejareja bali kwa vitendo vya kupunguza idadi ya wafanyakazi – jambo ambalo serikali haikutegemea.
Tatu, imekuza mapambano dhidi yake kwani wafanyakazi sasa wanaona kuwa serikali inataka kutumia mbinu ya kuwagawa kwa misingi ya sekta – binafsi na umma – ili kuwadhoofisha.
Profesa Kapuya na serikali wanakumbuka kuwa wakati fulani walitangaza nyongeza ya mishahara bila kushirikisha waajiri na waajiri, hasa wenye viwanda, wakakataa mapendekezo na amri za serikali.
Baadhi ya wenye viwanda walikuja na mapendekezo yao wakitaka serikali ikubaliane nao kwa mujibu wa maelezo kuhusu mapato, matumizi na matarajio ya viwanda.
Kama kuna wakati serikali iliumbuka na kudhalilika, basi ni wakati huo. Ilibidi waziri wa kazi afanye kazi ya ofisa wa uhusiano wa makampuni hayo – akieleza jinsi ambavyo viwanda havitamudu kulipa mishahara hiyo – na kufikia hatua ya kuweka viwango vipya.
Yote haya yamekuwa yakifanywa kwa kasi na bila kuwa makini kwa vile kwa kipindi kirefu serikali inadharau matakwa, wito na madai ya wafanyakazi. Hivyo inakurupuka hatua za lalasalama na kulazimika kutumia hata viinimacho.
Hata baada ya Rais Jakaya Kikwete kutoa kauli iliyofanana na kuwaangukia wafanyakazi, bado hakuna hatua za haraka zilizochukuliwa kukutana nao na kuwasikiliza kwa makini.
Tatizo kubwa ni kwamba watawala Tanzania, baada ya kurithishana madaraka kwa miaka yote hii – nusu karne – wamekuwa na tabia ya kuamini kuwa yanayosikika nchi za nje; ya wafanyakazi kugomea rais na serikali yake, hayawezi kufanyika hapa.
Hakuna wafanyakazi wenye musuli la vyuma. Hakuna wenye damu ya kijani. Kote duniani wafanyakazi wamekomazwa na mazingira yao.
Mahala pengi wamekomazwa na tabia na vitendo vya watawala. Bila kukohoa, kupaza sauti, kukemea, kukemea, kupanga na kupangua, kuandamana na kugoma, basi haki haipatikani.
Hilo ndilo linaunganisha wafanyakazi kote duniani: Kwamba kazi wanafanya lakini wananyonywa, wananyanyaswa na hawasikilizwi. Bila kuungana hawafiki popote.
Kwa njia hii huwezi kusema wafanyakazi wa Tanzania wana damu ya kijani na hivyo watakuwa na upole wa kondoo. Hapana.
Acha wasimame imara kudai chao. Wasipokipata leo watakipata kesho, mradi hawalazi msuli. Na kama serikali haitasikia leo, bila shaka itasikia kesho, na huenda katika mazingira tofauti na leo. Kapuya upoo?
0713 614872

KAWAWA NA 'USIMBA' WAKE
SITAKI
Wanaotaka kuzika ‘ujasiri’ wa Kawawa
Na Ndimara Tegambwage
SITAKI Watanzania wasahau Rashid Mfaume Kawawa; ingawa hakika watamsahau. Kama wamesahau Julius Kambarage Nyerere, sembuse “kibarua” wake.
Kawawa – Waziri Mkuu, Makamu wa Rais, Waziri Mkuu na Makamu wa Pili wa Rais na wakati huohuo Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, aliaga dunia juzi, Alhamisi akiuza uyoga.
Tusemezane. Tuambizane ukweli. Wakati aliyewahi kuwa na madaraka, nyakati hizo, ya kuumba na kuumbua anakufa akiuza uyoga, karani mmoja wa Benki Kuu (BoT) anajengewa nyumba kwa Sh. 1.4 bilioni.
Msanii wa viwango vyake, Kipanya, amefafanua nyumba ya karani wa BoT kama ifuatavyo: “Tumetumia bilioni moja point four tu kujenga my haus…Vere spesho haus. Ukija moto inajizima, yakija mafuriko inapaa.” Utaongeza nini hapa?
Pamoja na vyeo vyote alivyokuwa navyo, Kawawa hakuweza kujichotea mabilioni ya shilingi au kutumia nafasi yake kulainisha wahusika ili apate fedha za kufanyia biashara, kujenga nyumba za kifahari au kulalia katika mto (takia) au mfaliso. Wanasema kwa kejeli, “Yule alikuwa mjinga kama Nyerere kaka yake, au alimwogopa.”
Kwa hiyo katika mazingira haya, Kawawa aweza kusahaulika haraka. Hapana. Tuseme ukweli. Aliishasahaulika. Jina lake limerejeshwa na kifo chake; misururu ya kumuaga, kumzika na kutandaza unafiki wa kisiasa wa kutoa sifa kemkem kwa mtu ambaye uwezekano wake wa kuwakemea haupo tena.
Na atafutika haraka kweli. Hii ni kwa sababu Kawawa hakuandika vitabu. Hotuba zake hazikuhifadhiwa na kutungwa uzi na kuwa vitabu. Hakuandikwa sana na kufanyiwa utafiti kama Nyerere. Yeye hakuandika.
Juhudi za msomi mmoja ambaye hivi karibuni alitembelewa na busara za kuandika kitabu juu ya Kawawa, ni miongoni mwa watu wachache sana ambao wamehifadhi tunda la kichwa na mikono ya Kawawa.
Vinginevyo, Kawawa alikuwa mtekelezaji zaidi kuliko mwana-nadharia. Nyerere, ambaye aliamini na kuheshimu akiishasema, basi. Fikra au agizo linalotoka katika kichwa kinachoaminika kuwa sahihi, linapaswa kutekelezwa kuliko kufanyiwa porojo. Huyo ndiye Kawawa.
Kawawa hakuzalisha mawazo kwa njia ya nadharia. Alitenda. Alitekeleza kilichoamuliwa. Hakuwa na nia, sababu wala muda wa kurudia miito. Vyombo vya habari vilinukuu amri zake. Havikumchabua. Ama viliogopa, hasa wakati wa mfumo wa chama kimoja; au vilikuwa na ukame wa waandishi wenye upeo mkubwa.
Kuishia kudonoa na, au kuchambua maamuzi, sera, kanuni na taratibu; bila kujadili, kuchambua na kutafiti vitendo vya Kawawa, kumefanya mwanasiasa muhimu katika Tanzania kuwa na ukame wa fikra. Kumbe wenye ukame ni wale walioshindwa kutafsiri utendaji wake na kuupa nadharia.
Rashid Mfaume Kawawa hakutaka mjadala juu ya kilichoamuliwa. Alitaka utekelezaji. Hata pale Mwalimu Nyerere alipoonyesha kutoelewa au kutoafikiana na jambo fulani, yeye alikuwa wa kwanza kutenda, kwa njia ya kurekebisha, ili lifanane na Mwalimu alivyotaka.
Katika nyakati za mfumo wa chama kimoja na magazeti mawili – la serikali na la chama (TANU), ambako watawala walikuwa wakitumia kauli, “kama nchi tumeamua;” Kawawa, kama wanasiasa wengine, alisema chochote alichokuwa nacho huku akijiaminisha kuwa “vijana wetu” – waandishi wa habari – “watayaweka sawa.”
Ni nyakati hizo waandishi wa habari walitakiwa kujua viongozi wanataka kusema nini. Hata pale walipokosea kuelezea sera au siasa za nchi, mwandishi alitakiwa kuwa makini na kufafanua, kana kwamba ni yeye aliyekuwa anahutubia, msimamo na utashi wa serikali na kuweka wazi kuwa ndiyo hayo yaliyoelezwa na kiongozi, au Kawawa.
Chukua mifano hii. Nyerere aliongelea unyonyaji unaofanywa na wenye maduka na kueleza kuwa hali ingekuwa tofauti iwapo kungekuwa na maduka ya ujirani.
Palepale Kawawa alianza kwa kuamuru maduka ya watu binafsi yafungwe kwa kuwa yalikuwa ya “kinyonyaji.” Nchi ilitikisika chini ya kilichoitwa “Operesheni Maduka.” Bidhaa zikakosekana karibu na walipo wananchi. Haraka ya kutenda ambayo ilikuwa sura kamili ya Rashid Mfaume Kawawa. Ilichukua muda kurekebisha hilo.
Mfano wa pili. Waliokuwepo watakumbuka Kawawa alivyoamuru Umoja wa Vijana wa TANU kusimamia operesheni ya kuvaa nguo za heshima. Vijana wa kike waliovaa nguo fupi walikamatwa na baadhi yao kushikiliwa katika mazingira ya kutatabishwa yaliyoitwa “udhalilishaji.”
Kama siyo Nyerere kuingilia kati na kusema mavazi ni “fasheni tu” – zinakuja na kupotea, maisha mijini, na hasa Dar es Salaam, yalikuwa yameanza kuwa magumu kwa vijana wa kike. Lakini ni utekelezaji.
Chukua mfano mwingine wa kuhamia vijijini. Kawawa akiwa mtendaji mkuu, alitaka kila mmoja ahamie kwenye vijiji vilivyopimwa na alisisitiza sera hiyo kama ilivyoelezwa, kufafanuliwa na kuelekezwa na TANU na Baba wa Taifa Mwalimu Nyerere.
Ninajua vema kilichotendeka. Nilikuwa mwandishi niliyeshuhudia uhamishaji katika wilaya ya Kahama. Nyumba na maboma ya mifugo vilichomwa moto. Mifugo ilisambaa. Watu walisombwa kwa malori hadi “vijiji vilivyoandaliwa” ambako hakukuwa na nyumba bali kusanyiko la wengine waliosombwa kama mizigo.
Tukiwa katika ziara na Mwalimu Nyerere, mikoani Shinyanga na Mwanza, wananchi walijitokeza na kumwambia Mwalimu kuwa walitoka kwenye neema na kupelekwa kwenye majuto. Mzee mmoja aliyesimamisha msafara wa rais alisema, “Kuku wangu akitoka nje, tayari ameingia kwa jirani; sasa hapa ni kijiji kweli. Tunaishi kwa kugombana.”
Hata matatizo ya kuku, maji, nyumba alitwishwa Kawawa. Wakati Nyerere aliyezalisha mawazo alibaki shujaa wa kufikiri, msimamizi wa utekelezaji alivuna lawama na laana: Rashid Mfaume Kawawa.
Karibu sera zote za TANU na baadaye CCM, zilizojaa fikra fikirishi – kuanzia Azimio la Arusha – hazikuwa na mipango mkakati wala mipango ya utekelezaji. Ndiyo maana hata sera nzuri kama “Elimu ya Kujitegemea” ilikosa mwelekeo.
Miaka 20 baada ya Azimio la Arusha, kwenye kongamano la walimu wa siasa katika vyuo vya TANU, lililofanyika Chuo cha Kivukoni, Dar es Salaam, walimu walipoombwa kutoa maana ya elimu ya kujitegemea zilitokea tafsiri saba (7).
Walitofautiana juu ya utekelezaji kwa vile hawakuwa na mpango mkakati wala mpango wa utekelezaji. Yote haya alilundikiwa Kawawa. Mwalimu alifikiri, Kawawa alisimamia utekelezaji na kuvuna lawama.
Lakini Kawawa, kama Mwalimu Nyerere hawakukimbia matunda ya kazi zao. Nyerere ndiye alianzisha utaratibu wa kukiri makosa, hata kabla hajaulizwa, na kupendekeza masahihisho. Kwa njia hii alimnusuru “mpiganaji mwenzake” mara nyingi kabla hajalaumiwa, kushutumiwa na kulaaniwa.
Lakini Kawawa anakumbukwa kwa kile wengi wanaita “uaminifu.” Historia haionyeshi mahali popote ambapo Kawawa alionyesha jeuri kwa Nyerere; kupingana naye waziwazi au kumhujumu. Inaonyesha tumshikamano, kukubaliana na kutenda “bila swali.”
Huu ulikuwa woga au utii? Kuna majibu mengi kwa swali hili. Lakini kinachoonekana wazi na haraka ni kwamba kulikuwa na mshikamano wa kikomredi, kati ya Nyerere na Kawawa – kila mmoja akisema na kuapa kuwa “tunachofanya ni kitu chetu hadi mwisho.”
Sasa Kawawa hayupo nasi tena. Alazwe mahali pema anapostahili. Katika hili hatuna uamuzi. Bali kwa nini tusimkumbuke kwa haya machache – ujasiri wa kutenda hata pasipo na mpango kazi; urafiki na ukomredi usio na unafiki; na kutopenda makuu. Hivi havijafa.

SERIKALI NA SHERIA ZA KISHETANI
SITAKI
Sheria ya kishetani ya Waziri Mkuchika
Na Ndimara Tegambwage
SITAKI kuamini kwamba Waziri wa Habari, Utamaduni na Michezo, George Mkuchika anafanya kazi ya serikali. Hii ni kwa kuwa serikali nzima haiwezi kuwa na fikra finyu kiasi hiki. Haiwezekani.
Ijumaa iliyopita Mkuchika alitangaza kufungia gazeti la KuliKoni kwa siku 90. Waziri anadai gazeti limekiuka Sheria ya Usalama wa Taifa kwa kuandika “habari za jeshi.”
Waziri anasema “kosa” lilitendeka 27 Novemba 2009 pale gazeti lilipoandika juu ya kuvuja kwa mitihani ya jeshi na kuwepo uwezekano wa upendeleo kwa wasiostahili.
Mkuchika, kama Sheria ya Magazeti ya 1976 inavyosema, ana mahakama yake binafsi. Iko akilini mwake. Iko mikononi mwake. Iko mdomoni mwake. Anatamka kuwa habari iliyoandikwa na KuliKoni “ni ya uwongo.”
Ushetani wa Sheria ya Magazeti ni kwamba inasema anachosema waziri ndicho. Sheria iliyotungwa na binadamu mwenye kasoro na walakini kadha wa kadhaa, inampa waziri mamlaka ya kuumba na kuumbua, bila kupitia mahakamani.
Sasa Mkuchika anasema gazeti limesema uwongo. Hiyo ni katika mahakama ya akilini mwake kama alivyopewa mamlaka na sheria ya magazeti ambayo inamruhusu pia kufungia na hata kufuta gazeti bila kutoa sababu yoyote.
Kama kuna nchi ambako serikali zinaweza kuja na kupita na wakati huohuo kujiviringisha katika mazingaombwe na kuyarithisha kwa serikali zinazofuata, basi ni Tanzania.
Kwani kuwa na sheria ambayo inampa waziri uwezo wa kuamua anavyotaka, ni kufanya taifa kuwa la wanasesere wanaochezeshwa kwa vidolegumba.
Ukweli ni kwamba wengine – sisi – siyo wansesere. Hata kabla ya Tume ya Jaji Nyalali (1992) tulikuwa tumepaza sauti na kusema Sheria ya Magazeti ni ya kishetani; ni ya kishenzi.
Ripoti ya Tume ya Nyalali ilipokuja, ikaleta hoja kuwa sheria hiyo ama ifutwe au ifanyiwe marekebisho makubwa. Watawala wamekaa kimya. Wanaipenda. Wanaipakata. Wanampa Mkuchika aitumie atakavyo. Mkuchika anataka.
Ukiona watawala wanapenda sana sheria chafu, ujue kuwa roho, nia na shabaha zao ni chafu. Huwezi kulinda chema kwa kutumia sheria chafu. Huwezi kulinda kitakatifu kwa kutumia sheria ya kishetani. Utatumia sheria chafu kulinda kichafu. Huo ndio muwafaka. Mkuchika anataka.
Sisi, katika tasnia ya habari, tulianza kupaza zaidi sauti za kutaka sheria ya magazeti ifutwe tangu zaidi ya miaka 30 iliyopita. Ushahidi upo. Kila tulipopaza sauti ndivyo watawala walivyoweka sheria hiyo mbelekoni; kipenzi chao.
Leo KuliKoni imekumbwa na mkasa ulioikumba MwanaHALISI. Imefungiwa na Mkuchika kwa siku 90 kwa uamuzi wa waziri asiyependa kwenda mahakamani wala asiyeshawishi wahusika kwenda Baraza la Habari Tanzania.
KuliKoni imekumbwa na sheria inayoruhusu waziri kutumia utashi binafsi, mapenzi, chuki na hata husuda kufungia gazeti – mdomo wa umma. Mkuchika anataka sana.
Mkuchika anasema amelalamikiwa na jeshi. Jeshi lina uwezo wa kwenda kwenye Baraza la Habari na kulalamika. Jeshi linaweza pia kwenda mahakamani. Kwani jeshi ni nini kama siyo Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa? Waweza kulalamika popote.
Waziri Mkuchika hataki jeshi lihangaike. Hataki hata jeshi liunde Tume ya kuchunguza kama lilivyopendekezewa. Anakaa kitini na kusema gazeti limesema uwongo kwa kuwa sheria inamruhusu kuumba na kuumbua. Mkuchika anataka.
Taarifa ya gazeti, inayosema mfumo wa utungaji na ufanyaji mitihani ya kijeshi unawapa nafasi maofisa wasiostahili, inawezaje kuwa kitu cha kubomoa “usalama wa taifa?” Tangu lini usalama wa taifa umekuwa mweroro kiasi hicho?
Gazeti limetoka leo na malalamiko ya wahusika yanatoka siku hiyohiyo, hata kabla ya kuulizia wala kufanya uchunguzi. Kanusho la aina hiyo lina uzito gani?
Msajili ya Magazeti ni Mkurugenzi wa Idara ya Habari Tanzania (MAELEZO). Huyu anaamuru tu: “Jieleze kwa nini usichukuliwe hatua.” Basi. Yeye hafanyi uchunguzi angalu kupata mwanga na kusaidia walalamikaji.
Anaposema hakuridhika na kauli au majibu uliyotoa, ina maana kuwa ni suala la binafsi linalotokana na kutojua kinachoendelea au ni la kushinikizwa na aliyemlalamikia au woga tu kwamba jeshi limetajwa.
Katika mazingira haya, waziri anadai kuwa taarifa ya gazeti imefedhehesha “jeshi letu na kulipaka matope.” Mkuchika amepata wapi fedheha? Amepata wapi matope wakati hata aliyelalamika hajaweka ushahidi wake hadharani mbele ya chombo chenye hadhi ya kutoa maamuzi?
Hata katika suala la kujieleza; waziri anataka maelezo yenye ushahidi ili ayatumie wapi wakati yeye hafanyi uchunguzi wala hana chombo cha haki cha kutoa maamuzi?
Gazeti la MwanaHALISI bado lina kesi na serikali inayotokana na hatua ya Mkuchika kulifungia kwa siku 90 bila sababu ya msingi. Hapana, ni zaidi ya hapo.
Kuna kesi mahakamani, inayotafuta kufutwa kwa sheria ya magazeti. Haijaamuliwa. Ilichochewa na kufungiwa kwa MwanaHALISI na ndio walalamikaji.
Hata kabla kesi hiyo haijatolewa maamuzi, Mkuchika anaendeleza ubabe wake. Anaita taarifa za gazeti juu ya mitihani ya jeshi kuwa ni za “uchochezi” na analifungia kwa siku 90. Wako wapi wanasheria wa KuliKoni?
Huyo ndiye Mkuchika chini ya mwavuli wa serikali. Sheria ipo. Watawala wanaipenda. Mawaziri wanaoteuliwa huipenda, kuitii na kuinyenyekea kwa kuwa tatizo lao kuu ni “mlo.”
Hajapatikana waziri wa kukataa kutumia na kutumikia sheria chafu; angekuwa ametoa funzo. Hajapatikana wa kuasi utumwa wa sheria hii kwa kuwa wengi wanatafuta mlo.
Huwezi kutumikia umma ambao umeufunga mdomo. Basi huutumikii bali unausulubu katika utumwa wa mawazo na hatimaye katika vitendo. Utapataje mawazo yake? Utapataje malalamiko yake? Utapataje ushauri wake?
Ni heshima na halali, kwa waziri, msajili wa magazeti, maofisa wa habari serikalini, waandishi wa habari, wadau wengine wa habari na wananchi, kuasi sheria katili.
Kwa pamoja tunaweza kuvunja mikatale hii.
0713-614872
ndimara@yahoo.com
www.ndimara.blogspot.com
HAKUNA ADHABU YA KIFO: MUUAJI NI MUUAJI KAMA YULE WA KWANZA
SITAKI
Kunyonga siyo adhabu, ni kuua tu
Na Ndimara Tegambwage
SITAKI kuona wananchi na watawala wakishabikia hukumu ya kunyonga, hata kama kuna sheria ya nchi inayoruhusu mtu “kunyongwa hadi kufa.”
Sheria iliyopo ni katili, chovu, inayopaliliwa na kuendelea kurutubishwa na mfumo unaoendeshwa na watu ambao wamekuwa wagumu kuelewa mantiki ya thamani ya maisha na umuhimu wa adhabu.
Iwapo hawatakata rufaa, au wakikata rufaa na kushindwa, Masumbuko Madata, Emmanuel Masangwa na Charles Kalamuji, waweza kuuawa kutokana na hukumu iliyotolewa na Jaji Gabriel Rwakibalila.
Jumatano iliyopita, mjini Kahama, Jaji Rwakibalila aliwakuta vijana hao watatu na hatia ya jinai ya kuua Masumbuko Dunia, mtoto wa shule, umri wa miaka 13 na mwenye ulemavu wa ngozi (albino). Sasa kuna wanaoshangilia hukumu ya kifo.
Kifo cha Masumbuko kiliuma na kuumiza wengi, hata kama hawakuwa na uhusiano wowote naye. Umri wake mdogo; nafasi yake katika jamii iliyosababisha kuitwa majina ya kumtelekeza; utu wake ambao ulikuwa na bado ni sehemu ya utu wa kila mtu; ni sehemu tu ya chimbuko la uchungu.
Uchungu unakuwa mkubwa pale jamii inaposhuhudia mauaji yakilenga watu wenye ulemavu wa ngozi; wadogo kwa wakubwa, kwa sababu dhaifu, za kijinga na potofu – eti kupata viungo vya kuwawezesha “kuwa matajiri.”
Uchungu huu usio na udhibiti, unapokutana na sheria ambayo hata Jaji Mkuu Augustino Ramadhani amewahi kusema kuwa hafurahii kuitumia, ndipo unazaliwa ukatili mpya; ule wa kuondoa uhai wa aliyepatikana na hatia ya kuua.
Mahakama Kuu nchini Tanzania iliishawahi kutamka kuwa adhabu ya kifo ni ya kikatili na ya kudhalilisha na kutaka ifutwe. Pamoja na maeneo mengine, maneno “katili” na “kudhalilisha” ni ya msingi sana katika kuchambua hukumu ya kifo.
Katiba ya Jamhuri ya Muungano inakataza ukatili na udhalilishaji. Kwa hiyo kuwepo sheria inayoruhusu kuua; hivyo kuendesha “ukatili” na “udhalilishaji,” ni kuvunja katiba ya nchi. Lakini Mahakama ya Rufaa haikuafiki.
Hakuna ubishi kwamba vijana watatu wa Kahama, kwa kupatikana na hatia ya kumuua Masumbuko, walivunja haki za binadamu. Bali “haki za binadamu” haziwekwi na watu; zipo na zinahusu kila mmoja.
Watawala, sheria na hata Katiba za nchi, haziweki haki za binadamu. Ngazi zote hizo hazina uwezo wa “kugawia” watu haki za binadamu. Kinachofanyika ni kwa watawala, sheria na Katiba kutambua kuwepo kwa haki hizo na kutafuta jinsi ya kuzilinda na kuziendeleza.
Kwa hiyo, hapa siyo mahali pa hoja za jino kwa jino. Hoja ni kutovunja haki za binadamu. Kutoua. Kutofanya ukatili. Kutodhalilisha.
Hoja hii inaleta maana zaidi pale tunapojadili “thamani” ya adhabu anayopewa mkosaji. Watatu wa Kahama wamepatikana na hatia. Wamevunja haki za binadamu kwa kumuua Masumbuko. Wanastahili adhabu na ikiwezekana iwe adhabu kali.
Tujiulize. Je, hukumu inayoruhusu kifo ni adhabu? Je, kifo kinaweza kuwa adhabu? Je, adhabu hufanywa na aliyekufa? Kama sababu ya kuadhibu ni kutaka mtu ajirudi na kurejea katika utu wa jamii yake je, aliyeuawa anajirudi vipi, lini na wapi?
Hizi zinaonekana hoja ndogo kwa waliovimba vichwa na vifua, kwa hasira na uchungu wa kweli wa kupoteza watoto, ndugu, jamaa, rafiki au wenzao katika tabaka au kundi tambulishi kama walivyo albino.
Bali hasira zilizokaba koo za wafiwa; chuki zilizotunisha misuli ya shingo za ndugu wa aliyeuawa; na woga uliokumba nyoyo za wahusika; vyote vinaziba mifereji ya fikra kuhusu uhai wa mtu mwingine na nafasi ya muuaji mpya.
Vijana watatu wamepatikana na hatia ya kuua. Sheria inaruhusu wauaji kuuawa. Jaji, kwa mujibu wa sheria hajakosea kutamka hukumu hiyo kwa shabaha ya kulinda sheria na kazi yake. Bali Jaji aweza kuwa anaasi “shangazi wa mtima” wake.
Majaji wengi duniani wameeleza jinsi wanavyosutwa na dhamira zao pale wanapotamka hukumu ya kifo. Wameeleza jinsi kunavyokuwa na mapambano makali “rohoni” mwao na hatimaye kuanguka na kuwa mateka wa sheria na mfumo.
Leo kuna vijana watatu wa Kahama. Wanakabiliwa na mauti na siyo adhabu. Atakayeua vijana hao ni nani kama siyo muuaji?
Kuna tofauti gani kati ya aliyeua albino kwa panga na anayeua muuaji wa albino kwa kamba ya shingoni? Haipo. Wote ni wauaji. Mmoja anakanwa na sheria na mwingine anaruhusiwa na sheria. Wote wanatoa uhai wa watu wenye thamani ileile.
Ninaelewa ugumu wa wafiwa kuzingatia hoja hii haraka. Lakini malezi ya jamii hayawezi kwenda kwa misingi ya walioko madarakani kujipa fursa ya kuua na kujikinga na sheria walizotunga wenyewe.
Niliishawahi kuuliza katika safu hii wakati wa kujadili somo hilihili: “Kama serikali inaua, nani ataua serikali – ambayo sasa ni muuaji?” Sikupewa majibu.
Kuna haja ya kufikiri upya kuhusu sheria inayoruhusu kunyonga watu. Kunyonga ni kuangamiza maisha; siyo adhabu ya kurejesha mtu kwenye mstari wa maandili na utu wa wote.
Kunyonga ni kunyima aliyepatikana na hatia fursa ya mabadiliko katika maisha. Ni mabadiliko haya ambayo huweza kuwa mfano mkuu kwa jamii na kufanya watu wengi kukiri udhaifu wao na kuwa wanyoofu maishani.
Kuua hakuleti nafuu kwa mfiwa. Hakuna mafao kwa serikali. Hakuleti faida kwa jamii. Kunaendeleza vilio. Kunasimika hasira na chuki mpya. Kunafanya jamii ishindwe kuelewa nani anaweza kuikinga na ukatili huu.
Sheria zinazoruhusu mauaji kwa njia ya kunyonga ni za kuviziana; za kumalizana na mara nyingi, kama siyo mara zote, zinawaelemea wa tabaka la chini katika jamii. “Wakubwa” wana kila njia ya kuzipinda na hata kuzikatakata.
Sheria za kunyonga zinafanya jamii ianze kuona kuwa maisha hayana thamani. Zinafundisha usugu na kutothamini uhai binafsi na ule wa mtu mwingine. Zinazaa tabia ya “nitakuua hata kama wataniua.”
Sheria zinazoruhusu mauaji zinakomaza chuki na ghadhabu na zinafuta msamaha na tabia ya kujirudi ambayo ni nguzo kuu katika kupata suluhisho na muwafaka. Zinainyang’anya jamii ujasiri wa kufunza waliopogoka na kuikosesha jukumu la kufunza vizazi na vizazi.
Adhabu ilenge kurekebisha muhusika; kumfanya ajutie tendo lake na kutamani kurejea katika utu wake wa asili. Aliyekufa hajutii makosa yake; harekebiki pia.
Natamani kuona hukumu ya kifo ikifutwa na nafasi yake kwa sasa kichukuliwa na adhabu ya kifungo cha maisha. Aliyeua akiuawa, aliyeua muuaji anakuwa amekamilisha ukoo wa wauaji.
Katika ukoo huu, mauaji hayataisha. Hayataogopwa. Hayatapingwa kwa kuwa hayatachukiwa. Natamani yaishe. Jamii ivunje kimya.

POLISI NA MAUAJI YA SHELABELA YA WATUHUMIWA
SITAKI Na Ndimara Tegambwage
Polisi wanaoua vyanzo vya taarifa
SITAKI mauaji ya kila siku. Kila wiki. Kila mwezi na wauaji wakiondoka tu bila kukamatwa. Bila kuhojiwa. Bila kusutwa. Bila kukemewa. Bila kuchunguzwa.
Hii ndiyo wanaita tuumachi! Polisi wanachukua bunduki. Wanaangamiza roho ya mtu mmoja, wa pili, wa tatu, wa nne, wa tano. Wanakunja sime. Wanaondoka. Nisikilizie: Tumeua majambazi. Halafu? Kimya. Utadhani hakuna kilichotokea.
Taarifa za magazeti zimeeleza kuwa saa nane na nusu mchana; kweupe kabisa kwa tarehe 29 Novemba – wiki iliyopita tu – watu watano waliuawa katika kijiji cha Park Nyigoti wilayani Serengeti, katika mkoa wa Mara.
Eti polisi wakishirikiana na askari wa hifadhi ya mbuga ya Serengeti, waliwapiga risasi na kuwaua watu watano “wanaosadikiwa kuwa majambazi.” Ama walipiga mmojammoja au kwa risasi zilizotoka kwa mpigo; waliwateketeza wote fyuu!
Kama kawaida, polisi wakaondoka tu bila kujikamata. Bila kujihoji. Bila kujisuta. Bila kujikemea. Bila kujichunguza. Lakini pia bila kuhojiwa, kusutwa, kukemewa wala kuchunguzwa.
Ilikuwa 19 Novemba, wiki mbili na nusu zilizopita, watu sita waliuawa na polisi mkoani Dodoma. Hao pia “walisadikiwa kuwa majambazi.” Gun! Gun! Gun! Hadi sita. Polisi wakaondoka. Hawakujikamata, hawakujihoji, hawakujisuta wala kujichunguza. Vijana wanasema “imetoka hiyooo!”
Kama unataka maelezo juu ya ilivyotokea, sharti uwe unajua lugha na mwepesi wa kuchambua. Maneno yanayotumika ni istilahi maalum ya kipolisi: “Waliuawa wakati wa kujibizana kwa silaha na polisi.” Hayo ndiyo mazingira ambamo wanakufa wale wanaoshukiwa, wanaodhaniwa na, au wanaosadikiwa kuwa majambazi.
Siku sita baadaye, ilikuwa 25 Novemba, polisi waliripotiwa kuua kwa kupiga risasi, “majambazi” sita huko Biharamulo mkoani Kagera. Gun! Gun! Gun! Wote sita, chini. Taarifa zinasema walikutwa na silaha za moto.
Kama kawaida, hakuna polisi aliyekamata polisi kwa kuua. Hakuna aliyemhoji mwenzake. Hakuna aliyemsuta mwenzie. Hakuna mwenye nia ya kumchunguza mwenzake. Kimya. Utadhani umo kwenye tumbo la papa.
Kumekuwa na taarifa za kutupiana risasi, kati ya polisi na “majambazi” lakini kama ilivyo kwa sinema za Chuck Norris, mara zote hizi polisi ndio washindi – hawafi na kama wameumia sana, basi ni michubuko.
Mtindo huu wa polisi kuua “majambazi” au “wanaosadikiwa” kuwa majambazi au “wanaoshukiwa” kuwa majambazi hautalifikisha taifa hili popote katika vita dhidi ya ujambazi. Hatimaye polisi wataitwa wauaji tu. Ikitokea hivyo, hawataweza kujitetea.
Polisi aliyekabidhiwa bunduki ni yule aliyejifunza jinsi ya kuitumia kitaalam. Anapotumwa kwenye kazi ya kusaka majambazi, haendi au hapaswi kwenda kwa nia moja tu; kuua. Hapana. Kuna mambo mengi yanatarajiwa.
Polisi amefunzwa kulenga shabaha. Amefunzwa jinsi ya kutokuwa na kiwewe na harara katika mazingira ya “uwindaji” wa aina hiyo. Amefunzwa jinsi ya kurudi na ushahidi unaoongea ambao ni muhimu sana kwa mipango na operesheni za baadaye. Polisi hapelekwi tu kuua na kurejea na maiti.
Tena wajuzi wa kutumia silaha – wale wenye shabaha ya kuonea wivu – ndio wanahitajika sana; siyo kwa kupasua ubongo au moyo; bali kwa kupiga mguuni na takoni ili waweze kulegeza muhusika, kumkamata na kumhoji kwa manufaa ya kazi zao za baadaye.
Ni kweli polisi waliotumwa kazi waweza kujaa kiwewe na woga uliopindukia na kuanza kufyatua risasi hata bila kutumia utaalam waliopata vyuoni. Ni kutokana na uwezekano huo kunakuwa na haja ya kutaka kujua jinsi operesheni zinavyoendeshwa.
Ndio maana hata kwa upande wa polisi kuna haja ya kuulizana: Mbona mmeua wote? Mbona hamkuleta hata mateka mmoja? Mazingira yalikuwa vipi hadi mkaishia kuua tu? Ndio maana kuna haja ya kujikamata, kujihoji, kujisuta, kujikemea, kujichunguza na hata kujiadhibu.
Hivi ni kweli kwamba polisi wa Tanzania wanatumwa kuua tu? Hawataki mateka? Kama hawarudi na mateka watapata vipi taarifa za majambazi au wanaotuhumiwa kufanya ujambazi?
Gun! Gun! Gun! Watu 17 katika siku 20; ambao ni wastani wa kuua mtu mmopja kila siku; hakika hii haiwezi kuwa kazi bora ya polisi na hata ikilazimishwa kuwa, haiwezi kuwa na tija. Hii ni kwa kuwa hakuna maghala ya majambazi kiasi cha kufikiri kuwa jinsi wanavyouawa, ndivyo wanavyopungua katika maghala.
Uhalifu unamea katika ngazi mbalimbali katika jamii kwa vishawishi na motisha kadha wa kadhaa. Hapa umekomaa na kuwa wa matumizi ya kalamu ndani ya mabenki na serikali; pale umekomaa na kuwa wa matumizi ya silaha; pengine bado haujafumuka na labda kwingine ungali unasuasua.
Kwa hiyo, kuua raia kwa kuwa umemshuku au kwa kuwa amekutwa na silaha, hakusaidii polisi wala serikali. Moja ya kazi kubwa za heshima ambazo zinapaswa kufanywa na polisi, ni upelelezi.
Kupeleleza kunahitaji vyanzo vya taarifa. Vyanzo vizuri vya taarifa, hata kama itabidi taarifa hizo kuchambuliwa kwa makini sana, ni mateka na siyo wafu. Ukiua vyanzo vya taarifa na kurudi unajipiga kifua, utashindwa kumaliza uhalifu.
Kuua kunaweza kuwa na shabaha nyingine. Shabaha ya kuficha ushahidi muhimu. Ili waliouawa wasijulikane wana uhusiano na nani katika polisi, katika biashara au katika utawala.
Mauaji yakiendelea kwa miaka mingi yanakuwa njia ya kuondosha watu wasiokubaliana na polisi, watu mashuhuri au serikali. Katika baadhi ya nchi mauaji ya aina hiyo yamewakumba wapinzani wa watawala.
Hapo kuua huwa kunazoeleka na yeyote aweza kuokotwa kokote, kupelekwa Serengeti, Ngorongoro au hata Loliondo, kuuawa hukohuko na taarifa zikasambazwa kuwa “alikuwa mmoja wa majangili sita bali wengine aliokuwa nao wamekimbia.”
Kuruhusu polisi kuendelea kuua watuhumiwa wa ujambazi, kunaweza kuleta madhara zaidi kwa taifa. Kunajenga unyama usiomithilika nyoyoni mwa wauaji na woga miongoni mwa wananchi.
Kunadumaza utaalam katika idara ya upelelezi ambayo sasa inabakia kutegemea uvumi. Kwani, upelelezi hukomaa zaidi katika mazingira ya uhalifu na huimarisha nyanja mbalimbali za sheria ambako mbongo huchuana na kuweka misingi mipya ya kutafsiri sheria zilizopo na hata kutunga nyingine.
Kuendelea kuua watuhumiwa kunaharibu jina, sura na tabia ya nchi na wananchi – kwamba nchi na watu wake wanaitwa wauaji; lakini pia kunajenga mazingira ya kuviziana na hata mafisadi kutumia mwanya huo kuangamiza wasiowaabudu.
Kuua siyo njia bora ya kukabiliana na uhalifu. Hakika kuua kunaweza hata kuchochea uhalifu zaidi. Siku zote polisi waende kukamata, kupata vyanzo vya taarifa vya kuwasaidia katika uchunguzi na baadaye katika hatua za kukabiliana na ujambazi.
Penye mfumo mzuri wa matumizi ya polisi, mauaji ya watu watano, watano na baadaye sita, katika siku 20 tu, hayawezi kufumbiwa macho. Kama ndani ya jeshi la polisi na serikali hawaulizani “kulikoni,” basi wananchi wana kila sababu ya kuuliza.